Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 21:21

Kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana duniani kimeshuka kwa asilimia 13 mwaka 2023-Ripoti


Nembo ya shirika la kimataifa la kazi (ILO)
Nembo ya shirika la kimataifa la kazi (ILO)

Kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana ulimwenguni kilishuka kwa asilimia 13 mwaka 2023, kikiwa kiwango cha chini kwa kipindi cha miaka 15.

Lakini utafiti mpya uliofanywa na shirika la kimataifa la kazi unaonya kuwa kufufuka kwa uchumi baada ya janga la Covid 19 ni tofauti kutoka nchi hadi nyingine, huku baadhi ya maeneo yakishuhudia ongezeko la idadi ya vijana wasiokuwa na ajira.

ILO ilitoa ripoti yake ya mwaka 2024 kuhusu hali ya ukosefu wa ajira kwa vijana duniani kuambatana na siku ya kimataifa ya vijana Agosti 12, ili kuongeza ufahamu wa mahitaji, matumaini na matarajio ya vijana.

Ripoti ya sasa inazingatia masuala haya na kuchambua matarajio ya sasa na ya siku zijazo.

Ripoti hiyo inatabiri kuwa soko la ajira la kimataifa kwa vijana lililoimarika kwa kipindi cha miaka minne litaendelea na mwelekeo wake wa kuimarika zaidi kwa miaka miwili zaidi, huku viwango vya ukosefu wa ajira vikitarajiwa kushuka zaidi hadi asilimia 12.8 mwaka huu na ujao.

Forum

XS
SM
MD
LG