Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:44

Kituo maarufu cha reli cha Haramain huko Saudi Arabia kimewaka moto


Kituo cha treni ya mwendo kasi cha Al-Haramain kilichoungua huko Saudi Arabia
Kituo cha treni ya mwendo kasi cha Al-Haramain kilichoungua huko Saudi Arabia

Kituo hicho cha reli kilifunguliwa mwaka jana kinaunganisha miji miwili mitakatifu ya Mecca na Medina pamoja na mji wa Jeddah kwenye bahari ya Shamu. Ujenzi wake uligharimu dola bilioni 7.3 ambapo ni sehemu ya juhudi za kuongeza mapato ya utalii ya Saudi Arabia

Maafisa wa Saudi Arabia walisema Jumapili kwamba moto umewaka katika kituo cha reli ya mwendo kasi cha Haramain kilichopo pwani ya mji wa Jedda huko Saudi Arabia na kuwajeruhi takribani watu watano.

Kituo hicho cha reli kilichofunguliwa mwaka jana wa 2018 kinaunganisha miji miwili mitakatifu ya Mecca na Medina pamoja na mji wa Jeddah kwenye bahari ya Shamu.

Moshi mweusi ulitanda angani kutoka juu ya paa la kituo cha reli kwa kiasi cha masaa manne tangu tukio lilipotokea majira ya saa sita mchana kwa saa za huko, kulingana na picha zilizooneshwa kwenye Televisheni ya taifa ya Al-Ekhbariya. Taarifa ilieleza kitengo cha dharura kinachohusika na majanga kilipambana kuuzima moto huo.

Akaunti rasmi ya Twitter ya mji wa Mecca iliripoti kwamba watu watano walipelekwa hospitali wakiwa na majeraha. Ilieleza timu yenye wauguzi wa afya 16 ilikuwa ikifanya kazi katika eneo la tukio. Al-Ekhbariya ilisema watu wane walipatiwa huduma ya afya katika eneo la tukio.

Kituo hicho cha treni ya mwendo kasi kiligharimu dola bilioni 7.3 ni sehemu ya juhudi za kuongeza mapato ya utalii.

XS
SM
MD
LG