Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:51

Kisumu yaongoza kwa maambukizi mapya ya Covid 19


Mhudumu wa hospitali akimpima mtu mmoja COVID-19 katika maabara ya Kenya Medical Research Institute (KEMRI) huko Kisumu, magharibi mwa Kenya, Apr. 23, 2020.
Mhudumu wa hospitali akimpima mtu mmoja COVID-19 katika maabara ya Kenya Medical Research Institute (KEMRI) huko Kisumu, magharibi mwa Kenya, Apr. 23, 2020.

Mji wa magharibi mwa Kenya wa Kisumu umeupita mji mkuu Nairobi, kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya COVID-19 nchini humo. Kuongezeka kwa kesi hizo kumekuja siku moja baada ya kiongozi wa upinzani kuhutubia umati mkubwa huko Kisumu, ambapo pia waliripoti kesi ya kwanza ya Covid kutokana na virusi vipya kutoka nchini India.

Kwa mujibu wa wizara ya afya, kaunti ya Kisumu inarekodi idadi kubwa ya visa vya COVID-19.

Jiji la Lake side siku ya Jumanne lilirekodi karibu theluthi moja ya visa 382 vilivyorekodiwa nchini humo. Waziri wa Afya wa kaunti ya Kisumu Boaz Otieno anasema mlipuko huo umeongezeka kwa zaidi ya siku 10 zilizopita au zaidi.

“Sisi ni eneo kuu la maambukizi hadi sasa. Tuna zaidi ya kesi 4,000 ambazo zimethibitishwa hadi kufikia mwisho wa wiki iliyopita, karibu 3,000 au zaidi kidogo kati ya hizo ziligunduliwa katika siku saba zilizopita.”

Otieno pia analaumu ongezeko la Kisumu linatokana na kupungua vikwazo katika mji mkuu wa Nairobi na maeneo ya kuzunguka.

Amesema “kulikuwa na utitiri wa marudio yasioweza kuepukika. Kwa kawaida kuna muingiliano wa shughuli nyingi za watu kati ya Kisumu, Nakuru na Nairobi. Kwa hivyo kama ukiwa unawafungia watu na kisha unawaachilia kwa kawaida tabia ya watu kujitokeza kwa kasi na kurudi majumbani”.

Mwishoni mwa Machi, Rais Uhuru Kenyatta alizuia harakati za watu jijini Nairobi na katika kaunti za Kajiado, Nakuru, Kiambu na Machakos katika jaribio la kuzuia kuongezeka kwa visa vya COVID-19. Rais alipunguza vizuizi mwezi mmoja baadaye.

Ongezeko la maambukizo linakuja wakati Kaunti ya Kisumu ikijiandaa kuandaa sherehe ya Siku ya Uhuru Juni mosi ambayo Kenyatta anatarajiwa kuhudhuria.

Wiki mbili zilizopita, Kisumu ulikuwa mji wa kwanza nchini Kenya kurekodi kesi yenye aina virusi kutoka India. Otieno alisema hakuna cha kuwa na wasiwasi juu yake na itifaki za kiafya zitafuatwa wakati wa sherehe hiyo.

Waziri wa Afya wa Kenya Mutahi Kagwe alisema Jumanne kuwa watu wasiopungua 950,000 nchi nzima walipewa chanjo dhidi ya virusi vya corona. Taifa hilo la Afrika Mashariki limerekodi visa 169,000 vya COVID-19 na zaidi ya vifo 3,000 kutokana na ugonjwa huo.

XS
SM
MD
LG