Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:14

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine asema amewekwa chini ya kizuizi cha nyumbani


Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na mgombea wa zamani wa urais Bobi Wine leo Alhamisi amesema polisi waliizingira nyumba yake na kumuweka “chini ya kizuizi cha nyumbani” kabla ya maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika.

Wanasiasa wa upinzani walikuwa wamepanga maandamano dhidi ya barabara mbovu sana nchini Uganda, ambayo ni mwenyeji wa mikutano miwili ya kimataifa katika siku zijazo.

Wine, mwanamuziki aliyegeuka kuwa mwanasiasa, amesema polisi na wanajeshi wamemzuia kuondoka nyumbani kwake huko Magere, kaskazini magharibi mwa mji mkuu Kampala.

“Jeshi na polisi wameizingira nyumba yetu na kutuweka chini ya kizuizi cha nyumbani lakini maandamano yanaendelea,” kiongozi huyo wa chama cha National Unity Platform (NUP), alisema kwenye mitandao yake rasmi ya kijamii.

Wine, ambaye jina lake la kweli ni Robert Kyagulanyi alishindana na Rais mkongwe Yoweri Museveni kwenye uchaguzi wa mwaka 2021, akiomba kumalizika kwa utawala wa kimabavu wa Museveni.

Mgombea wa zamani wa urais Kizza Besigye wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change amesema leo kuwa yeye pia hakuruhusiwa kuondoka nyumbani kwake.

Forum

XS
SM
MD
LG