Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:48

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal ashtakiwa kuongoza uasi, chama chake chafutwa


Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko (Katikati), wakati wa mkutano wa chama chake mjini Dakar, Machi 13, 2023.
Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko (Katikati), wakati wa mkutano wa chama chake mjini Dakar, Machi 13, 2023.

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko Jumatatu alishtakiwa kwa kuongoza uasi na chama chake kikafutwa, hali ambayo ilisababisha mapambano kati ya waandamanaji na polisi.

Sonko, mgombea urais na mkosoaji mkubwa wa Rais Macky Sall, amekabiliwa na msururu wa kesi, ambazo anadai ni za kujaribu kumtenga kwenye uwanja wa siasa.

Hukumu dhidi yake ya kifungo cha miaka miwili jela bila mwenyewe kuwepo mahakamani ambayo ilitolewa mwezi uliopita katika kesi ya utovu wa maadili ilichochea mapambano ambayo yalisababisha vifo vya watu 16 kulingana na serikali, vifo vya watu 24 kulingana na Amnesty International, na vifo vya watu 30 kulingana na chama cha Sonko cha PASTEF.

Lakini hajafungwa jela licha ya hukumu hiyo.

Siku ya Ijumaa, alikamatwa kwa tuhuma mpya zinazohusiana na maoni aliyotoa, mikutano ya hadhara aliyofanya na makosa mengine tangu mwaka wa 2021.

“Nimewekwa chini ya ulinzi wa polisi kinyume cha sheria,” Sonko mwenye umri wa miaka 49 aliandika kwenye ukurasa wa Facebook Jumatatu alasiri.

Chini ya saa mbili baada ya kufunguliwa mashtaka, waziri wa mambo ya ndani alitangaza kwamba chama cha Sonko cha PASTEF kitavunjwa “kwa kuchochea mara kwa mara” uasi, na kusababisha uharibifu na vifo.

Forum

XS
SM
MD
LG