Anaonekana akiwaambia wanajeshi wake kwamba watakaa kwa muda fulani Belarus kupewa mafunzo ya kijeshi kabla ya kupelekwa barani Afrika.
“Karibuni. Nafurahi kuwasalimu nyote. Karibuni kwenye ardhi ya Belarus”, video ilimuonyesha akisema.
“Tulipigana kwa heshima. Tumeitendea mengi Russia,” aliongeza.
Uasi wa Prigozhin, ambao ulikuwa tishio kubwa zaidi kwa utawala wa miaka 23 wa Rais Vladimir Putin, ulielezewa na kiongozi huyo wa mamluki kuwa ulilenga kuwaondoa viongozi wakuu wa jeshi la Russia ambao aliwashtumu kuwa wazembe.
Ukosoaji wa Prigozhin juu ya uendeshaji wa mapigano nchini Ukraine ulirudiwa katika video hiyo mpya, ambayo uhalisi wake haukuweza kuthibitishwa mara moja.
“Kinachoendelea kwenye uwanja wa mapigano leo ni aibu ambayo hatupaswi kuhusishwa nayo,” alisema, akiongeza kuwa wanajeshi wa Wagner wanaweza kurejea Ukraine katika siku zijazo.
Forum