Hiyo ni sehemu ya muendelezo wa maelewano ya kidiplomasia ambayo yalihusisha kupeana zaidi mikono, kujiburudisha na baadhi ya vinywaji vya Korea wakati wa chakula cha mchana na furaha ya pamoja ya kuangalia timu "zilizoungana" za Korea zikicheza mchezo wa hockey wakati wa michezo ya Olympic ikiwa katika siku ya pili huko Korea Kusini.
Hakuna kilichoamuliwa na Rais wa Korea Kusini kuhusu mualiko huo lakini iwapo utafanyika itakuwa ni wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi baina ya nchi hizo mbili.
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Moon amesisitiza umuhimu wa kuwepo mkutano huo na ameeleza hatua hiyo ya Korea Kaskazini kurejea katika meza ya mazungumzo na Marekani.
Ujumbe huo wa mdomo uliotolewa kwa "wakati unaostahili" kutoka kwa dikteta Kim Jong Un, uliwasilishwa na dada mdogo wa Kim Yo Jong, ni sehemu ya hatua za haraka za kuboresha hisia kati ya pande mbili zenye mvutano wakati wa michezo ya Olympic ya Pyeongchang.