Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 21, 2024 Local time: 23:22

Kiongozi wa kidini Fethullah Gulen amefariki akiwa na umri wa miaka 83


Fethullah Gulen akiwa nyumbani kwake huko Saylorsburg katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani.
Fethullah Gulen akiwa nyumbani kwake huko Saylorsburg katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani.

Gulen alikuwa mshirika wa Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan lakini walitofautiana na aliwajibishwa kwa jaribio la mapinduzi la 2016

Kiongozi wa kidini Fethullah Gulen mwenye makao yake nchini Marekani, ambaye aliunda vuguvugu lenye nguvu la Kiislamu nchini Uturuki na kwingineko, lakini alitumia miaka yake ya karibuni akishutumiwa kwa kupanga jaribio la mapinduzi dhidi ya kiongozi wa Uturuki Tayyip Erdogan, amefariki dunia. Alikuwa na umri wa miaka 83.

Herkul, tovuti ambayo inachapisha mahubiri ya Gulen, ilisema kwenye akaunti yake ya mtandao wa X kwamba Gulen alifariki Jumapili jioni katika hospitali moja ya Marekani ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Gulen aliwahi kuwa mshirika wa Erdogan lakini walitofautiana, na Erdogan alimwajibisha kwa jaribio la mapinduzi la mwaka 2016 ambapo wanajeshi wahuni katika nafasi za juu waliongoza ndege za kivita, vifaru na helikopta.

Takriban watu 250 waliuawa katika juhudi za kutaka kukamata madaraka. Gulen ambaye alikuwa akiishi uhamishoni nchini Marekani tangu mwaka 1999, alikanusha kuhusika na shambulio hilo lakini kundi lake lilitajwa kuwa kundi la kigaidi na Uturuki.

Forum

XS
SM
MD
LG