Makundi hayo yanaungwa mkono na Islamic State kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na mkutano huo.
Mwanajihadi huyo ni Iyad Ag Ghaly, mwenye asili ya Ki-Tuareg ambaye anaongoza kundi la GSIM, ambalo limekuwa likipambana na kundi lililojitangaza na lenye ushawishi ndani ya Sahel la Islamic State.
Siku za hivi karibuni amekuwa akifanya mikutano kaskazini mwa Mali, ikijumuisha na viongozi wa makundi ya wenye silaha ambayo yamekuwa yakipambana kwa vita kali na kundi la wanajihadi la Islamic State kwa mujibu wa chanzo.
Wamethibitisha kuhusu kufanyika kwa mazungumzo, lakini hawakutoa maoni yoyote kutokana na tetesu zinazo ongezeka kwamba GSIM itajiunga na makundi hayo.