Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:35

Kimbunga Freddy chaua mamia na kuathiri maelfu ya watu


Maiti ikipakiwa kwenye gari la wagonjwa wakati wa uokoaji huko Blantyre, Malawi, Machi 17, 2023. Picha na Amos Gumulira / AFP.
Maiti ikipakiwa kwenye gari la wagonjwa wakati wa uokoaji huko Blantyre, Malawi, Machi 17, 2023. Picha na Amos Gumulira / AFP.

Kimbunga Freddy, ambacho kilitoweka wiki hii, baada ya kuvunja rekodi, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 400 katika maeneo ya kusini mwa Afrika na kuathiri zaidi ya watu nusu milioni nchini Malawi, Umoja wa Mataifa umesema Ijumaa.

Dhoruba hiyo ilisababisha mvua ya miezi sita kwa muda wa siku sita katika eneo la kusini mwa Malawi, na kuacha mlolongo wa uharibifu ukiwemo uharibifu mkubwa wa miundo mbinu pamoja na mashamba kufurika.

"Zaidi ya watu 500,000 wameathirika – wakiwemo watu 326 waliopoteza maisha wakati zaidi ya watu 183,100 wamekoseshwa makazi," ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema katika ripoti.

Ripoti hiyo imeonya kuwa takwimu hizo zinatarajiwa kuongezeka katika siku zijazo nchini humo yenye karibu watu milioni 20.

"Mfumo wa hali ya hewa uliovunja rekodi uliikumba Malawi mwishoni mwa msimu wa mvua wakati mito na vyanzo vya maji vilikuwa tayari vimejaa," OCHA ilisema.

Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Paul Turnbull siku ya Ijumaa alisema ni dhahiri kwamba nchi hiyo "itahitaji msaada mkubwa".

Turnbull amesema, maeneo mengi ni vigumu kufikiwa “yanazuia timu kufanya tathmini na hali ya kibinadamu na ufikishaji vifaa vya kuokoa maisha."

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amesema hadi sasa, serikali imetaja idadi ya watu waliopoteza makazi yao ni zaidi ya 183,000, na pia ameomba msaada wa kimataifa ili kukabiliana na mahitaji ya kibinadamu.

Chanzo cha habari ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG