Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 22:19

Kikosi maalum cha dharura cha EU kubuniwa


Mku wa sera za kigeni wa EU Josep Borrell akihutubia kikao cha wanachama kwa njia ya kimitandao
Mku wa sera za kigeni wa EU Josep Borrell akihutubia kikao cha wanachama kwa njia ya kimitandao

Mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya, EU Alhamisi wamefanya kikao cha kujadili namna nzuri ya kukabiliana na mizozo katika siku za usoni  baada ya Taliban kuchukua udhibiti wa Afghanistan,ikiwemo kubuni kikosi maalum cha kukabiliana na dharura.  

Wakati wa kikao hicho kllichofanyika Slovenia,walijadili kuhusu walichojifunza kutokana na vurugu za kuondoka Afghanistan baada ya Taliban kukamata nchi, wakati Ujerumani ikipendekeza kwamba wanachama wa EU wabuni kikosi maalum cha wanajeshi 5,000, kitakachoweza kukabiliana na dharura bila kuitegemea Marekani.

Suala hilo limekuwa kwenye ajenda ya EU kwa zaidi ya muongo mmoja, lakini yalioshuhudiwa Afghanistan hivi karibuni yamepelekea mataifa yote 27 wanachama kulijadili kwa haraka. Mkuu wa sera za mambo ya nje kwenye EU Josep Borrell amesema Alhamisi kwamba anatumai mpango huo utakamilika ifikapo mwezi Novemba. Ameongeza kusema kwamba ni dhahiri sasa kwamba sasa kikosi hicho kinahitajika kwa haraka kufuatia yalioshuhudiwa Afghanistan.

Kuchukuliwa kwa Afghanistan na Taliban pamoja na dharura ya kuokoa maelfu ya watu kwa njia ya ndege baada ya Marekani kuamua kuondoa vikosi vyake nchini humo , kumeonyesha utegemezi mkubwa wa EU kwa Marekani.

Ingawa vikosi vya EU vilikuwa vikisaidiana na Marekani wakati wa kuokoa watu, Marekani kwa sehemu kubwa iisaidia mataifa ya EU kuhamisha watu wake.

XS
SM
MD
LG