Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 04:12

Kijana wa Israel akutwa amekufa Ukingo wa Magharibi


Mwili wa kijana wa Kiisraeli aliyetoweka umepatikana Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na walowezi Jumamosi, katika kile Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, amekiita mauaji ya kutisha.

Kutoweka Ijumaa kwa Benjamin Achimeir, mwenye umri wa miaka 14 kuliibua msako mkubwa na mashambulizi dhidi ya vijiji vya Wapalestina.

Waziri mkuu Netanyahu, amesema katika taarifa yake kwamba mauaji ya kinyama ya kijana huyo ni uhalifu mkubwa. Vikosi vya Israel, viko katika msako mkali kutafuta wauwaji na wale walio shirikiana nao.

Achimeir, alitoweka mapema Ijumaa kutoka kituo cha nje cha Malachi Hashalom karibu na mji wa Ramallah.

Mwili wake ulipatikana karibu jeshi la Israeli, vikosi vya usalama vimesema.

Maelfu ya Waisraeli wanaishi katika makazi ya Ukingo wa Magharibi yanayochukuliwa kuwa si halali chini ya sheria za kimataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG