Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:52

Kijana aliyetekeleza mashambulizi ya risasi Serbia amekamatwa


Wanfunzi wakiomboleza kuuawa kwa wenzao wakiwa shuleni, Serbia. May 4, 2023
Wanfunzi wakiomboleza kuuawa kwa wenzao wakiwa shuleni, Serbia. May 4, 2023

Polisi nchini Serbia wamemkamata mtu anayeaminika kuwaua watu wanane na kujeruhi wengine 14 kwa kuwapiga risasi, kabla ya kwenda mafichoni.

Mtu huyo alifanya mashambulizi ya bunduki wakati akiendesha gari lake, jana Alhamisi.

Mauaji ya Alhamisi ni ya pili katika muda wa siku mbili. Yamefanyika siku moja baada ya kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 13 kufaya shambulizi katika shule moja huko Belgrade na kuua watu tisa na kujeruhi wengine 7.

Kulingana na shirika la habari la Serbia RTS, Polisi wamemkamata mshukiwa huyo ambaye alitoroka baada ya shambulizi.

XS
SM
MD
LG