Rais mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki, Jumatano amekabiliwa vyeti vyake baada ya kuteuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni. UNESCO miezi miwili iliopita mjini kwenye makao yake makuu mjini Paris, Ufaransa.
Wakati wa uteuzi huo mwezi Aprili,mkurugenzi wa UNESCO ,Irina Bovoka alisema kazi ilioifanya nchini Kenya na barani Afrika ya kuhamasisha kuhusu utumizi wa Maji na umuhimu wa Elimu inaendelea kutambuliwa na Shirika lake.
Wakati wa hafla hiyo iliofanyika mjini Nairobi, na iliohudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu Serikali na vile vile mashirika mbali mbali, Kibaki alishukuru Umoja wa Mataifa kwa kutambua juhudi zake za kutunza vyanzo vya maji nchini. Kwa habari zaidi zikiliza habari ilitayarishwa na mwandishi wa VOA Kennedy Wandera akiwa Nairobi.