Wajumbe wa baraza la mji wa DC waliungana na wanaharakati wa Saudia Arabia katika kubadilisha jina la barabara mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia na kuweka jina la “Jamal Khashoggi Way”.
Phil Mendelson, mwenyekiti wa Baraza la DC alieleza haya: “ Baraza lilipiga kura kwa sauti moja kubadilisha jina la mtaa huu, mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia, kwa sababu tunataka kukumbuka na kuweka kumbukumbu ya muathiriwa wa ukandamizaji na kumshukuru kwa kuzungumza.”
Kashoggy aliyekuwa na umri wa miaka 59 , mwandishi wa habari maarufu wa Saudi Arabia na makala za Washington Post, aliingia katika ubalozi wa Saudia Arabia kutafuta nyaraka muhimu kwa ajili ya mpango wa kumuoa mchumba wake aliyekuwa anamsubiri nje. Hakuonekana tena.
Saudi Arabia ilikataa kuhusika na kutoweka kwake.
Baadae shirika la kijasusi la Marekani lilitoa ripoti likisema kwamba Kashoggy aliuwawa na kukatwa vipande vipande kwa amri ya mwanamfalme wa Saudia Mohammed Bin Salman.