Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 11:49

Kesi ya uhalifu wa vita dhidi ya Bemba inaanza The Hague


Kiongozi wa chama cha upinzani MLC, Jean-Pierre Bemba akipiga kura Kinshasa, DRC 2006.
Kiongozi wa chama cha upinzani MLC, Jean-Pierre Bemba akipiga kura Kinshasa, DRC 2006.

Kesi ya uhalifu wa vita dhidi ya makamu rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jean Pierre Bemba, imeanaza The Hague, Uholanzi kwenye Mahkama ya Uhalifu wa Kimataifa, ICC.

Anashtakiwa kwa makosa matatu ya uhalifu wa vita na mawili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu ulotendwa jamhuri ya Afrika ya Kati na wapiganaji wake wa kundi la MLC, kati ya 2002 na 2003.

Akizungumza mbele ya mahakama wakati wa kufunguliwa kesi Jumatatu, mwendesha mkuu wa mashtaka wa ICC Luis Moreno-Ocampo amesema kesi hiyo itaamua ikiwa kamanda huyo anawajibika kisheria kwa ukatili ulofanywa na wapiganaji wake.

Moreno-Ocampo anasema, "Sisis katika afisi ya mwendesha mashtaka hatusemi kwamba Jean-Pierre Bemba alitenda uhalifu huo binafsi, hajambaka mwanamke yeyote. Sisi hatusemi aliamrisha. Bali tunachosema hakua na udhibiti wa wapiganaji wake na hiyo ni jukumu la kamanda."

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, iliwasilisha mashtaka hayo mbele ya ICC 2004. Wakosowaji wanashuku na mashtaka hayo wakidai kwamba Rais Ange-Felix Patasse ndiye aliyemualika Bembe kumsaidia kuzima uwasi nchini mwake.

Geraldine Mattioli-Zeltner wa Human Rights Watch ameiambia Sauti ya Amerika kwamba, kwa vile Bemba haja tuhumiwa kutenda uhalifu huo mwenyewe, inaifanya kesi kua ngumu lakini pia muhimu sana.

Huko DRC wafuasi wake sawa na wananchi wa kawaida wanataka kesi imalizike haraka maana hawafahamu kwanini awajibike kwa kitu ambacho hakukifanya..

XS
SM
MD
LG