Barrow alishinda tena kwenye uchaguzi wa Decemba 4 kwa asilimia 53 ya kura zilizopigwa akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu Ousainou Darboe kwa asilimia 28 ya kura, wakati wagombea wengine wawili wakipinga matokeo kwa madai kwamba kulikuwa na dosari kwenye vituo vya kupigia kura, bila kutoa ushahidi.
Kwa mijibu wa shirika la habari la Reuters, chama cha Darboe cha United DiplomaticUDP,kiliwasilisha ombi la kufutwa kwa zoezi hilo, kwenye mahakama ya juu kwa madai kwamba halikufanyika kwa njia ya haki. Hata hivyo mahakama imesema kwamba chama hicho hakikuwasilisha malalamishi hayo ndani ya siku 5 kwa Barrow kama inavyohitajika kwenye sheria za Gambia.