Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 15:29

Mahakama Kuu Kenya yasema Uhuru alichaguliwa kihalali


Uhuru Kenyatta alichaguliwa kihalali, mahakama yasema
Uhuru Kenyatta alichaguliwa kihalali, mahakama yasema

Mahakama kuu ya Kenya imetangaza Jumamosi kuwa Uhuru Kenyatta alichaguliwa kihalali katika uchaguzi mkuu uliopita Kenya. Uamuzi huo unatolewa wiki kadhaa baada ya uchaguzi kufuatia hatua ya mpinzani wake Raila Odinga kupinga matokeo hayo na kufungua madai mahakama kuu. Mahakama kuu imesema Jumamosi, kwamba uchaguzi ulikuwa huru na halali.

Wakenya wamekuwa wakisubiri uamuzi wa mahakama kwa shauku kubwa. Polisi Ijumaa ilitoa ilani kwa wafuasi wa pande zote mbili kujiepusha na kushereheka au kulalamika kufuatia uamuzi wa mahakama.

Kulingana na ratiba Uhuru Kenyatta ataapishwa rasmi kuchukua uongozi wa Kenya Aprili 9, 2013.

Kiasi cha saa moja na nusu baada ya uamuzi wa mahakama Raila Odinga alihutubia taifa akikubali uamuzi wa mahakama na kutoka wito kwa Wakenya kuwa watulivu na kukubali matokeo.

Odinga alimtakiwa rais mteule Uhuru Kenyatta uongozi mwema na kuitakia Kenya heri na fanaka.

XS
SM
MD
LG