Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 11:24

Kenyatta akosoa uamuzi wa mahakama wa kutupilia mbali kesi ya Odinga


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) akisalimiana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga. Nairobi, March 9, 2018. Kenyatta amemuunga mkono Odinga katika uchaguzi wa mwaka 2022 lakini akashindwa na William Ruto. Picha: Reuters
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) akisalimiana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga. Nairobi, March 9, 2018. Kenyatta amemuunga mkono Odinga katika uchaguzi wa mwaka 2022 lakini akashindwa na William Ruto. Picha: Reuters

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameahidi kuhakikisha kwamba anakabidhi madaraka kwa uongozi mpya, wa Dr. William Ruto.

Katika ujumbe uliorekodiwa na kuwekwa kwenye mtandao wa You Tube, Kenyatta hata hivyo ameonekana kukosoa uamuzi wa mahakama ya juu uliotupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa William Ruto.

Kesi hiyo iliwasilishwa na Raila Odinga wa muungano wa Azimio. Kiongozi mkuu wa muungano wa Azimio ni rais Uhuru Kenyatta.

“Hatua ya kukabidhi madaraka imeanza, ikisimamiwa na kamati iliyoundwa kufanikisha shughuli hiyo, na iliyoanza kazi Agosti tarehe 10. Nia yangu ni kuhakikisha kwamba shughuli ya kupokezana madaraka inafanyika kwa njia nzuri kabisa,” amesema Uhuru.

Hotuba ya Uhuru haijamtaja Ruto wala kumtumia ujumbe wa kheri njema, lakini anataka “wakenya kudadisi zaidi uamuzi wa mahakama ya juu uliotupilia mbali kesi ya Raila Odinga”.

Amedai kwamba “uamuzi wa mahakama haulingani na matarajio ya wakenya kuhusu uchaguzi wa urais na matokeo yake”.

Taasisi za kikatiba zinastahili kujaribiwa

Uhuru amesema kwamba ni “jukumu la kila mkenya kudadisi kwa undani kabisa na kutafuta ukweli kuhusu maamuzi yanayofanywa na taasisi za kikatiba na kuzifanyia majaribio ili kuhakikisha kwamba maamuzi yanayotolewa ni sawa”.

“Je, inahusu hesabu au namna ya kufikia hesabu hiyo? Mchakato huo unafuata kanuni za demokrasia? Je, taasisi inaweza kutoa maamuzi yanayotofautiana kuhusu jambo moja katika mazingira tofauti bila kuchunguzwa?” ameendela kuuliza maswali katika video iliyowekwa kwenye mtandao.

Kenyatta amesema kwamba uamuzi wa mahakama haulingani na uamuzi uliotolewa mwaka 2017, mahakama hiyo ilipofutilia mbali ushindi wake.

Mahakama ya juu ya Kenya ilifutilia mbali ushindi wa Uhuru Kenyatta mwaka 2017 baada ya Raila Odinga kuwasilisha ushahidi kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na dosari chungu nzima.

Uhuru Kenyatta amemuunga mkono Raila Odinga katika uchaguzi wa mwaka huu 2022 licha ya ahadi aliyokuwa ametoa kwamba angemuunga mkono naibu wake Dr. William Ruto wakati anapomaliza muda wake wa mihula miwili madarakani.

XS
SM
MD
LG