Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 02:19

Kenyatta aidhinishwa kugombea urais Kenya


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya awahutubia wafuasi wake kwenye eneo la Donholm, mjini Nairobi kabla ya kuwasilisha makaratasi yake kwa tume ya IEBC tarehe 29 Mei 2017.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya awahutubia wafuasi wake kwenye eneo la Donholm, mjini Nairobi kabla ya kuwasilisha makaratasi yake kwa tume ya IEBC tarehe 29 Mei 2017.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, siku ya Jumatatu alikabidhiwa hati ya kugombea urais na tume ya uchaguzi na mipaka ya Kenya, IEBC, baada ya kuwasilisha stakabadhi zake kwa tume hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Kenyatta International Convention Center, mjini Nairobi.

Kenyatta atawania urais kwa tikiti ya chama kinachotawala cha Jubilee.

Kiongozi wa muungano wa upinzani, Raila Odinga, alikabidhiwa hati yake siku ya Jumapili kwenye ukumbi huo huo. Odinga anasimama kwa chama cha ODM chini ya muungano wa NASA.

Wagombea wengine pia walisilisha makaratasi yao na kuidhinishwa, huku wengine wakikatiziwa azma yao ya kuwa rais kwa sababu ya dosari mbali mbali.

Baadaye, rais Kenyatta alihutubia mkutano kwenye bustani za COMESA grounds.

Mpinzani wake mkuu, Raila Odinga, alihutubia wafuasi wake kwenye uwanja wa Donholm, mjini Nairobi siku ya Jumapili.

Tume hiyo iliwaidhinisha wawaniaji tisa wa urais, wengi wao wakiwa ni wagombea huru.

Kipindi kilichotengwa cha kampeni nchini Kenya kilianza rasmi hiyo jana, na kitaendelea hadi tarehe tano mwezi Agosti, siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu.

XS
SM
MD
LG