Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:53

Vikosi vya Kenya vimewaua al Shabaab 31 Somalia


Vikosi vya Kenya vinavyoshiriki katika AMISOM
Vikosi vya Kenya vinavyoshiriki katika AMISOM

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters nchi hiyo ya Afrika Mashariki ina maelfu ya wanajeshi wake katika Kikosi cha Umoja wa Afrika (AMISOM) vinavyoendelea kupambana na al Shabaab.

Vikosi hivyo pia vimeendelea kuboresha hali ya usalama ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuijenga upya Somalia baada ya miongo mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo iangamiza nchi hiyo.

“Majeshi ya ardhini yalisaidiwa na mashambulizi yaliyofanywa na helikopta na makombora,” KDF imesema katika taarifa yake kuhusu shambulizi hilo la Jumapili katika vituo vya al Shabaab kwenye wilaya ya Baadhade huko Jubbaland.

Majeshi ya Kenya pia yamekamata silaha, zikiwemo bunduki aina ya AK 47, vifaa vya mawasiliano, uniform, imesema KDF.

Kenya ilipeleka vikosi vyake Somalia mwaka 2011 baada ya mashambulizi kadhaa yaliofanywa na al Shabaab katika ardhi ya Kenya na vikundi vya al Qaeda venye mafungamano na al Shabaab.

XS
SM
MD
LG