Gavana wa benki kuu ya kenya Kamau Thugge amesema leo jumatano kwamba nchi yake inatarajia kupata mkopo mpya wa karibu dola bilioni moja kutoka Uchina mnamo mwaka huu wa fedha na inaweza kutumia fedha hizo kulipa deni lake la Eurobond ambayo inatarajiwa kuanza kulipwa mwezi june mwakani.
Mkopo huo ulitangazwa kwa mara ya kwanza na maafisa wa kenya mwezi Oktoba ikionesha mabadiliko ya msimamo wa serikali ya Rais William Ruto kuhusiana na kukopa kutoka China baada ya kukosoa mikopo wakati wa kampeni zake wakati wa uchaguzi wa mwaka jana.
Thugge ameuwambia mkutano wa waandishi habari hii leo jumatano kwamba benki kuu iko kwenye majadiliano na serikali ya Chijna hivi sasa juu ya mkopo huo lakini muda wa kuupokea haujaamuliwa bado. Amesema wanatarajia kuupata mkopo kabla ya june 2024 na utatumiwa kwa ajili ya kuanza kulipa mkopo wa Eurobond.
Forum