Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 00:49

Kenya: Viongozi wa dini wanataka wanasiasa kujiepusha na matamshi ya chuki


Wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga wakiwasha moto barabarani jijini Nairobi, Kenya March 27, 2023
Wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga wakiwasha moto barabarani jijini Nairobi, Kenya March 27, 2023

Viongozi wa kidini na makundi ya haki za kibinadamu nchini Kenya wametoa wito wa utulivu baada ya wiki ya pili ya maandamano dhidi ya kupanda kwa gharama ya Maisha ikiongeza hofu ya uwezekano wa vurugu zaidi.

Wito huo umetolewa huku rais wa Kenya William Ruto akisema kwamba wahalifu watawajibishwa.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, ambaye alishindwa katika uchaguzi wa mwezi Agosti, anaongoza maandamano dhidi ya kuongezeka kwa gharama ya Maisha. Amewataka wafuasi wake kujitokeza kila jumatatu na alhamisi ili kuishinkiza serikali ya Ruto kuchukua hatua.

Watu wasiojulikana walichoma moto kanisa na biashara kadhaa, jumattu usiku, katika mtaa wa Kibera ni eneo la watu wa kipato cha chini. Msikiti pia uliharibiwa.

Mtu mmoja alipigwa risasi na kufariki katika mji wa Kisumu, karibu na nyumbani kwake Odinga.

Watu wasiojulikana walivamia shamba la rais mstaafu Uhuru Kenyatta na kuhairbu mali. Uharibifu pia uliripotiwa katika kampuni ya Raila Odinga. Kenyatta alimuunga mkono Raila Odinga katika uchaguzi wa mwaka uliopita.

Polisi wamesema kwamba wanachunguza matukio hayo huku wafuasi wa serikali na wale wa upinzani wakishutumiana kwa mashambulizi hayo.

viongozi wa kidini wameonya vurugu zinaweza kugeuka na kuwa mapigano ya kikabila kama yale yaliyotokea nchini humo mwaka 2007, ambapo zaidi ya watu 1000 waliuawa.

Wamewataka wanasiasa kujizuia kutoa matamshi ya uchochezi ambayo yamepelekea uharibifu kufikia sasa.

Rais wa Kenya William Ruto, akiwa Ujerumani, amesema kwamba maandamano ni changamoto kwa demokrasia ya nchi hiyo, akiapa kulinda mali na Maisha ya wakenya. Ameonya kwamba wahusika wote wa uhalifu watawajibishwa bila kujali nafasi yao katika jamii.

XS
SM
MD
LG