Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:26

Kenya yasaidia majeruhi wa Somalia


Baadhi ya watu waliojeruhiwa Mogadishu wakisubiri kusafirishwa Uturuki. Wengine wamepelekwa Kenya.
Baadhi ya watu waliojeruhiwa Mogadishu wakisubiri kusafirishwa Uturuki. Wengine wamepelekwa Kenya.

Ubalozi wa Somalia nchini Kenya pamona na shirika la Red Cross, na serikali ya Kenya,mapema Jumanne walizindua mpango wa kusaidia wahanga wa shambulio la kigaidi lililowaua watu zaidi ya 300 mjini Mogadishu,Somalia.

Mpango huo ni pamoja na uzinduzi wa namba maalum ya kuchangisha pesa kutoka kwa wahisani, na dawa za kuwatibu manusura.

Waziri wa masuala ya nje wa Kenya Amina Mohamed ametangaza kuwa Kenya imetuma ndege mbili Mogadishu zikiwa na tani 31 za dawa.

Mlipuko wa bomu kwenye lori ulitokea Jumamosi
Mlipuko wa bomu kwenye lori ulitokea Jumamosi

Ndege hizo zinatazamiwa kuwasafirisha hadi Nairobi majeruhi takriban 20, watakaopokelewa na hospitali za Kenya.

Utoaji wa damu kwa hiari ili kuwasaidia wahanga hao wa shambulio la bomu, umekuwa ukiendelea Jumanne hii katika eneo la Estleigh,Nairobi lenye watu wengi wa asili ya Kisomali.

Majeshi maalum ya Kikosi cha AMISOM nchini Somalia pia yalizindua zoezi kama hilo la kutoa damu kwa hiari, katika mji wa Mogadishu.

Misaada zaidi ya matibabu na upkoaji imetolewa na mataifa ya Djibouti, Turkey na Marekani.

Shambulio la bomu Jumamosi lililowaua watu zaidi ya 300 na kujeruhi wengine wengi, limetajwa kama mbaya zaidi nchini Somalia katika miongo miwili iliyopita.

XS
SM
MD
LG