Wakati wiki hii kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis anatarajiwa kuzuru Kenya, misafara ya waumini imeshuhudiwa kutoka mikowani hadi mji mkuu Nairobi ambako kiongozi huyo atakutana na wakenya.
Mji wa mombasa umeripotiwa kuwa na msafara mkubwa zaidi, na jana walikuwepo kwenye maombi maalum yaloandaliwa na muungano wa dini mbali mbali nchini Kenya.