Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:54

Kenya yapata vifaa vya kisasa vya polisi


uhuru azindua vifaa vya kisasa vya polisi
uhuru azindua vifaa vya kisasa vya polisi

Na BMJ Muriithi

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, siku ya Jumatatu alizindua rasmi vifaa vya kisasa vya kutumiwa na idara ya polisi nchini humo. Vifaa hivyo vilikuwa ni pamoja na magari yaliyo na silaha ambayo alisema yatatumiwa katika maeneo yanayokumbwa na ukosefu wa usalama nchini humo.

Akizungumza mjini Nairobi alipowakabidhi rasmi maafisa wa ngazi za juu vifaa hivyo, Kenyatta alisema hatua hiyo itawawezesha maafisa wa polisi kutotegemea vifaa vya jeshi la taifa kila kunapotokea hali ya taharuki inayohitaji polisi kuingilia kati.

Magari yanayomilikiwa na polisi wa Kenya
Magari yanayomilikiwa na polisi wa Kenya

"Ununuzi wa vifaa hivi ni hatua muhimu katika kupambana na utovu wa usalama," alisema rais Kenyatta.

Haya yanajiri takriban wiki tatu tu baada ya wanajeshi ambao idadi yaka bado haijajulikana kuuawa baada ya shambulizi lililotekelezwa na magaidi ya Al Shabaab katika kambi ya El-Ade, nchini Somalia.

XS
SM
MD
LG