Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:04

Kenya: Mabaki ya ndege yapatikana, 10 wapoteza maisha


Mabaki ya Ndege iliyopotea siku ya Jumanne nchini Kenya, yamepatikana Alhamisi katika msitu wa Aberdares, ulioko takriban Kilomita 130 Kaskazini mwa mji wa Nairobi.

Kampuni inayomiliki Ndege hiyo imesema kuwa watu wote waliokuwemo, wamekufa.

Ndege hiyo, aina ya Cesna, ilikuwa imebeba watu 10, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wawili na abiria nane.

Ndege hiyo ilikuwa inatoka Kitale ikielekea Nairobi Jumanne jioni, wakati ilipotoweka kwenye mitambo ya mawasiliano wakati ikiwasiliana na uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, ambako ilikuwa inatarajiwa kutua.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ametuma salamu za rambirambi kwa jamaa wa waathirika wa ajali hiyo na kusema kwamba serikali itatoa msaada kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.

XS
SM
MD
LG