Gazeti rasmi la serikali lililotolewa Jumatatu Februari 13, 2023 jeshi la taif KDF litatumwa kupambana na wezi wa mifugo wenye silaha katika sehemu za Turkana, West Pokot, Elgeyo Marakwet, Baringo, Laikipia na Samburu.
Rais wa Kenya William Ruto ameahidi kupambana vilivyo na kuhakikisha kwamba kuna utulivu na tatizo la wizi wa mifugo linasuluhishwa.
Seikali imetoa muda wa siku tatu kwa wezi wa mifugo, ambao wamejihami kwa silaha, kujisalimisha na silaha zao kuchukuliwa na maafisa wa usalama.
“Ni lazima tufanye kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba kuna usalama katika sehemu zenye matukio ya wizi wa mifugo. Tutafanya kila tunaloweza kuwaondoa wahalifu wote,” amesema rais William Ruto wakati wa mkutano na viongozi kutoka kaunti ya Baringo, uliofanyika katika ikulu ndogo ya rais mjini Nakuru.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wabunge kutoka sehemu zenye vifa vya wizi wa mifugo.
Rais Ruto ameelekeza Jeshi la Kenya KDF kufanya kazi kwa ushirikiano na polisi kukabiliana vilivyo na wezi hao wa mifugo.
Watu 12 wakiwemo maafisa wa polisi 7 wamelazwa hospitalini wakiwa na majeraha ya risasi baada ya kushambuliwa na wezi wa mifugo.
Kamanda wa polisi wa sehemu hiyo ni miongoni mwa waliojeruhiwa.
Magari mawili ya polisi pia yamechomwa moto baada ya polisi waliokuwa wanapiga doria Ijumaa wiki iliyopita kushambuliwa.