Bondia Rayton Okwiri wa Kenya alishinda mechi yake ya kwanza katika uzito wa Welter weight na kuwa mfano kwa mabondia wengine wa Kenya baada ya kumshinda Andrei Zamkovoi wa Russia.
Okwiri sasa ataingia katika raundi ya pili na mshindani ambaye bado hajajulikana.
Okwiri alipata ushindi wa pointi 2-1 kutoka kwa majaji baada ya raundi taut. Ushindi wa Okwiri bila shaka utawatia hamasa mabondia wengine wa Kenya katika michuano ya ndondi ya Olimpiki. Peter Mungai na Benson Gicharu ni mabondia wengine wa Kenya ambao wataingia ulingoni baadaye.