Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 21:03

Katibu Mkuu UM aitaka Israel kusitisha mashambulizi Syria


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Alhamisi alitoa mwito kwa Israel kusitisha mashambulizi yake ya anga dhidi ya Syria, akiyataja kuwa ni ukiukaji wa mamlaka ya nchi hiyo na uadilifu wa himaya. 

“Utawala wa Syria, umoja wa eneo na uadilifu lazima urejeshwe kikamilifu, na vitendo vyote vya uchokozi lazima vikomeshwe mara moja,” Guterres aliwaambia waandishi wa habari.

Toka serikali ya Rais Bashar al-Assad, wa Syria, ilipoanguka ghafla mapema mwezi huu, Israel imefanya mamia ya mashambulizi ya anga, ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Damascus, ambayo inasema yanalenga kuharibu silaha za kimkakati na miundombinu ya kijeshi.

Familia ya Austin Tice, mwandishi wa habari wa Marekani aliyezuiliwa nchini Syria kwa zaidi ya miaka 12, imeibua wasiwasi kwamba huenda Israel ikapiga sehemu ya nchi ambayo mwandishi huyo anaweza kuwepo ameshikiliwa.

Forum

XS
SM
MD
LG