Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 08:13

Kasisi na waumini wake wameuwawa kanisani Burkina Faso


Burkina Faso
Burkina Faso

Shambulizi hilo limetokea siku mbili baada ya wanajeshi wa kikosi maalumu cha Ufaransa kuwaokoa mateka wanne raia wa kigeni huko kaskazini ya nchi katika shambulizi la usiku kucha ambalo lilisababisha vifo vya wanajeshi wawili.

Watu wenye silaha wamemuua padri mmoja na waumini watano wakati wa sala ya Jumapili katika shambulizi kwenye kanisa katoliki kwenye mji wa Dablo, kaskazini mwa Burkina Faso.

Vyanzo vya usalama na ofisa kwenye mji huo walieleza kwamba washambuliaji waliwasha moto jengo la kanisa hilo pamoja na majengo mengine jirani na hapo ikiwemo kituo cha huduma za afya.

Meya wa mji wa Dablo, Ousmane Zongo aliliambia shirika la habari la AFP kwamba kundi la washambuliaji 20 hadi 30 waliwashambulia waumini na kuzusha hali ya taharuki katika mji huo.

Wanajeshi zaidi kutoka Barsalogho kiasi cha kilomita 45 kusini ya Dablo walipelekwa na kuanza msako mara moja. Hili ni shambulizi la tatu katika muda wa wiki chache zilizopita dhidi ya makanisa.

Shambulizi hilo limetokea siku mbili baada ya wanajeshi wa kikosi maalumu cha Ufaransa kuwaokoa mateka wane raia wa kigeni huko kaskazini ya nchi katika shambulizi la usiku kucha ambalo lilisababisha vifo vya wanajeshi wawili.

António Guterres, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
António Guterres, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

​Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alilaani shambulizi hilo la Jumapili na alitoa salam za rambi rambi huku akikumbushia kuheshimu sehemu zote za kuabudu, kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake. Guterres aliwasihi raia wote wa Burkina Faso kusimama imara na kusaidiana kila mmoja katika kipindi hiki kigumu katika juhudi za kusitisha ghasia zaidi.

XS
SM
MD
LG