Sherehe zimeanza katika mji mkuu wa Libya kufuatia ripoti kwamba kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Moammar Ghadafi amefariki kotokana na majeraha aliyopata wakati wa mapigano makali katika mji alikozaliwa wa Sirte.
Mapema Alhamisi viongozi wa kijeshi wa serikali ya mpito ya Libya NTC wailitangaza kukamatwa kwa Kanali Gadhafi baada ya kujeruhiwa vibaya kutokana na mapigano ya bunduki alipokuwa anajaribu kukimbia kutoka mji huo.
Inaripotiwa kwamba mwenyekiti wa NTC Mustafa Abdel Jalil anatarajiwa kulihutubia taifa hivi punde, wakati ripoti zikienea ikiwa kweli kiongozi huyo wa muda mrefun amefariki au amejeruhiwa na anashikiliwa na serikali ya mpito. Hakuna habari huru za kuthibitisha ripoti hizo zote.