Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 00:53

Kampuni zinazosambaza nishati ya jua zinasemekana kuwa miongoni mwa zinazokua kwa kasi zaidi Afrika


Kijana mmoja akiwa amesimama kando ya kituo cha nishati ya jua inayofadhiliwa na NGO ya Ujerumani huko Ghana, Septemba 6, 2024. (Picha za AP/Abdul Haqq Mahama).
Kijana mmoja akiwa amesimama kando ya kituo cha nishati ya jua inayofadhiliwa na NGO ya Ujerumani huko Ghana, Septemba 6, 2024. (Picha za AP/Abdul Haqq Mahama).

Kampuni zinazosambaza nishati ya jua kwa baadhi ya kaya maskini zaidi huko Afrika ya Kati na Magharibi zinasemekana kuwa miongoni mwa zinazokua kwa kasi zaidi Afrika

Kampuni zinazosambaza nishati ya jua kwa baadhi ya kaya maskini zaidi huko Afrika ya Kati na Magharibi zinasemekana kuwa miongoni mwa zinazokua kwa kasi zaidi katika bara ambalo serikali zake zimekuwa zikihangaika kwa muda mrefu kushughulikia baadhi ya miundombinu mibaya zaidi duniani na matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Bei huanzia chini ya dola 20 kwa taa inayotumia nishati ya jua hadi maelfu ya dola kwa vifaa vya nyumbani na mifumo ya burudani.

Afrika ya Kati na Magharibi ina viwango vya chini zaidi vya usambazaji wa umeme. Huko Afŕika Maghaŕibi, ambapo watu milioni 220 wanaishi bila umeme, hii ni chini kiasi cha asilimia 8 kwa mujibu wa Benki ya Dunia. Wengi hutegemea zaidi mafuta ya taa ghali na mafuta mengine yanayojaza nyumba na biashara mbali mbali moshi na hatari ya kusababisha moto.

Forum

XS
SM
MD
LG