Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:17

Kaimu mkurugenzi wa VOA atangaza mabadiliko ya uongozi


Michael Pack mkurugenzi mtendaji wa USAGM
Michael Pack mkurugenzi mtendaji wa USAGM

Kaimu mkurugenzi wa Sauti ya Amerika Elez Biberaj anasema, anarudi katika nyadhifa aliyokua nayo katika VOA wakati mkurugenzi mtendaji wa shirika mama la vyombo vya habari vya umma Marekani, USAGM, Michael Pack ateua viongozi wepya.

Elez Biberaj aliyetangazwa kaimu mkurugenzi wa Sauti ya Amerika mwezi June, alituma ujumbe wa barua pepe kwa wafanyakazi Jumanne usiku akieleza kwamba muda wake katika nafasi hiyo unamalizika na akimtakia mkurugenzi mpya mafanikio katika kutekeleza malengo ya VOA.

USAGM haijatangaza bado nani atachukua nafasi ya Biberaj, lakini kabla ya kutoa ujumbe wake Jumanne usiku, msemaji wa VOA alisema kwamba Biberaj bado ni "kaimu mkurugenzi."

Vyombo vya habari vya Marekani hata hivyo, vimeripoti kwamba mkurugenzi wa zamani wa VOA Robert Reilly, mwandishi na mwanadiplomasia aliyekua mkurugenzi wa VOA kati ya 2001-2002, ndie ameteuliwa.

Reilly ameshachapisha makala akimunga mono Pack. USAGM imekata kujibu maombi ya barua pepe kuzungumzia juu ya nani atachukua nafasi ya Biberaj.

Elez Biberaj akizungumza kwenye mkutano huko Tirana, Albania
Elez Biberaj akizungumza kwenye mkutano huko Tirana, Albania

Mwezi uliyopita haji mmoja wa mahakama ya serikali kuu aliamua kwamba baadhi ya hatua alizochukua Pack kama Mkurugenzi Mtendaji zina kiuka Kifungu cha Kwanza cha haki za waandishi habari wa shirika hili. Jaji alimarisha Pack kutoingilia kati kazi za kufuatilia babami za VOA na kusitisha uchunguzi wa jinsi habari zinavyoandikwa. Pack hata hivyo anaendelea kua na mamlaka ya kumteua mkurugenzi mpya wa VOA.

Katika barua yake pepe kwa wafanyakazi, Biberaj alisema kwamba, miezi sita iliyopita imekua yenye changamoto zaidi kuliko wakati wowote mnamo historia ya karibuni ya VOA. Aliandika kwamba," baadhi ya maafisa wa idara hawajaheshimu kanuni, itifaki na utaratibu ambao anachukulia si mambo yakukiuka."

Biberaj alisema atarudi katika nyadhifa yake ya zamani kama mkurugenzi wa idhaa ya Ulaya na Asia.

Rais Donald Trump alimteua Michael Pack zaidi ya miaka miwili iliyopita kua mkurugenzi mtendaji wa USAGM inayosimamia Sauti ya Amerika, Radio Free Asia, Radio Free Europe na mashirika mengine ya habari za kimataifa.

XS
SM
MD
LG