Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:31

Kagame azikosoa nchi za Magharibi


Rais Paul Kagame
Rais Paul Kagame

Rais Paul Kagame wa Rwanda Ijumaa ameyakosoa mataifa ya magharibi kwa kushinikiza mfumo wa demokrasia yao katika bara la Afrika.

Ametoa wito kwa nchi za Afrika kutafuta suluhisho la matatizo ya Afrika wao wenyewe.

“Ninapenda kuchukua fursa hii kuwashukuruni kwa sababu nchi za Kiafrika mmekuwa pamoja na Rwanda wakati tulipowahitajia mno,” amesema Rais Kagame.

Vyanzo vya habari vimesema kuwa Kagame amesema kuwa kuwepo kwa ndugu wa kiume na wakike kutoka Afrika nzima katika sherehe hizo za kuapishwa inalipa heshima ya dhati “taifa letu na kutuongezea nguvu.”

Akihutubia maelefu ya wananchi wa Rwanda na wageni waalikwa katika hafla ya kuapishwa kuwa rais, Kagame ameeleza kuwa kuchaguliwa kwake tena kwa naawamu ya tatu inatosheleza kuonyesha jinsi wananchi wa Rwanda wanavyo jiamini na kuahidi kuwa hatawaangusha katika kipindi chake kipya ya miaka saba.

Wale waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Kagame ni pamoja na marais Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Omar al-Bashir wa Sudan, Salva Kiir Mayardit wa Sudan Kusini, Ali Bongo wa Gabon, Idriss Déby Itno wa Chad na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Rais Alpha Conde of Guinea.

Wengine ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi. Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania hakuhudhuria. Lakini Magufuli alikuwa amewakilishwa na Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin. Alisafiri na ndege ya rais mpaka Kigali.

XS
SM
MD
LG