Katika mahojiano siku ya Alhamisi Kabwe alikosoa msimamo wa Rais Magufuli wa kukataa kufunga shughuli zote za biashara na utawala katika miji ambayo kuna uambukizaji mkubwa zaidi kama vile Dar es Salaam, kama wanavyofanya nchi nyingine duniani.
Akiwahutubia viongozi wa usalama nchini siku ya Juamtano Rais Magufuli alisema," wapo wengine wanatoa mawazo ya kuifunga Dar es Salaam, hili haliwezekani. Dar es salam ndio centre pekee ambapo collection ya revenue inapatikana kwa nchi yetu"
Kiongozi wa ACT Mzalendo anasema kwamba ni kweli kuna baadhi ya nchi ambazo haziwezi kusitisha shughuli zote za kiuchumi, lakini kulingana na Benki Kuu ya Dunia, "Tanzania inauwezo wa kufunga shughuli kwa kiwango fulani na serikali ikawafidia wananchi na kuwalipa."
Anasema akiba ya fed za kigeni ya Tanzania inaweza kutosha kuendesha nchi kwa zaidi ya miezi sita bila ya shughuli zozote kufanyika.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC