Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 06:46

Kabila azindua miradi ya ujenzi wa miundo mbinu Butembo


Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo

Rais Joseph Kabila amezindua ujenzi wa barabara muhimu katika mji wa Butembo, mashariki ya Congo katika lengo la kuleta maendeleo na kudumisha amani na ustawi.

Akiwa katika ziara ya kutembelea maeneo ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemnokrasia ya Kongo, Rais Joseph Kabila alizindua siku ya Jumatatu ujenzi wa barabara kuu katika mji wa Butembo ikiwa ni moja wapo ya miradi ya ujenzi wa miundo mbinu katika eneo hilo.

Akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi, Rais Kabila alisema licha ya miradi hiyo cha muhimu ni kudumisha amani."Tunachohitaji ni kusimamisha vita ambavyo vilikua vinataka kuvuruga kabisa biashara katika Kivu ya Kaskazini. Ahadi niliyotoa kwa wananchi wote wa Kivu ya Kaskazini kwangu mimi ni deni, na hilo deni mimi nitalilipa", alisema rais Kabila.

Licha ya juhudi hizo kunawatu wasio ridhika na kazi hizo wakidai kwamba kilicho muhimu zaidi ni kuhakikisha usalama na utulivu katika eneo hilo kabla ya kuanzishwa miradi kama hiyo.Mwakilishi wa chama cha upinzani cha MLC huko Butembo anasema kunafaida gani ya kutembea kwenye barabara ya lami wakati hakuna usalama.

Lakini viongozi wa jimbo la Kivu ya Kaskazini wanaishukuru serikali ya Kinshasa kwa miradi hiyo ambayo wanasema itasaidia sana kuimarisha usalama na amani pamoja na kuleta maendeleo. Msemaji wa gavana wa jimbo hilo Celestin Siboman Kapitula anasema hii ni dalili kwamba amani imeweza kurudi na hivyo hivi sasa kuna nafasi ya kuleta maendeleo katika eneo hilo.

XS
SM
MD
LG