Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 19:35

Kabila akaa kimya juu ya kugombea awamu ya tatu


Rais Joseph Kabila
Rais Joseph Kabila

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila Ijumaa ameendelea kusema nchi yake itafanya uchaguzi ulioahirishwa katika muda uliopangwa pamoja na kuwepo shinikizo linalomtaka ajiuzulu kabla ya uchaguzi huo.

“Ni lazima uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa,” Kabila asema katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu 2012, na kueleza kuwa uchaguzi huo utafanyika Disemba 23, 2018 kama ilivyotangazwa 2017.

“Nafahamu kuwa kwa upande wetu kuna muongozo na kile watu wengine wanachojaribu kupendekeza ni maneno matupu, wanarukia kitu kisichokuwepo na kuchechemea kwenda kusikojulikana.

“Nitapenda wote kwa pamoja tuhakikishe kuwepo uchaguzi wa amani. Je, hilo ndilo upinzani unataka—alihoji?” alisema katika tamko lake la kisiasa.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa katika mkutano usio wa kawaida na waandishi kwa masaa mawili, Kabila alitoa kauli ya ufunguzi ambayo ilifuatiwa na maswali na majibu.

Lakini Kabila hakujibu swali la msingi iwapo atagombania katika awamu ya tatu—kitu ambacho kimepigwa marufuku na katiba.

Kabila,46, ameshikilia madaraka tangu mwaka 2001, katika kipindi ambacho utawala wake umekosolewa kwa kuwepo ufisadi, ukandamizaji na uzembe.

Muda wake wa kuongoza kikatiba ulimalizika Disemba 2016 lakini akabakia madarakani, chini ya sheria zinazomruhusu kubakia katika wadhifa wake mpaka mrithi wake atakapo chaguliwa.

Chini ya mazungumzo ya kutafuta suluhu yaliyofanyika Disemba 31, 2016 yakisimamiwa na kanisa Katoliki, Kabila alikubali kufanyika uchaguzi mpya ifikapo mwisho wa mwaka 2017.

Lakini serikali ya Kongo mwisho wa mwaka 2017 iliahirisha uchaguzi hadi Disemba 23, 2018, ikidai kuwa kulikuwa na matatizo ya matayarisho ya uchaguzi.

Tangia wakati huo kumekuwepo na maadamano kadhaa yakimtaka aachie madaraka, na yamekuwa yakizimwa na vyombo vya usalama vya nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG