Kikosi hicho kinapitia wakati mgumu kusaidia polisi wa Haiti kudhibiti magenge yenye silaha ambayo yanawatishia raia, huku baadhi ya mataifa yakitaka kubadilisha kikosi cha kimataifa kuwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa.
“Bila ya ongezeko kubwa na endelevu la michango ya hiari kutoka kwa nchi wanachama, kuna hatari ya MSS kutokuwa na vifaa kamili, kutumwa kikamilifu au kuweza kuendeleza uungaji mkono wake kwa polisi wa Haiti,” Miroslav Jenca, msaidizi wa katibu wa Umoja wa Mataifa, aliwaambia wajumbe wa Baraza la Usalama kwa kutumia kifupi cha ujumbe wa Msaada wa Usalama wa Kimataifa.
Alisema misheni hiyo inahitaji ongezeko kubwa la silaha, vifaa na utaalam maalum ambao polisi wa Haiti hawana.
Forum