Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 07:17

Jumuiya wa kimataifa inaahidi kuboresha mgogoro wa wakimbizi


Mkutano wa Umoja wa Mataifa unaozungumzia suala la wakimbizi duniani
Mkutano wa Umoja wa Mataifa unaozungumzia suala la wakimbizi duniani

Jumuiya ya kimataifa inaahidi kuboresha uwajibikaji wake kwa mgogoro wa wakimbizi na wahamiaji duniani, japokuwa kuna maswali kadhaa iwapo mpango unakidhi vya kutosha.

Kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa Jumatatu, nchi wanachama zilikubaliana kulinda haki za wakimbizi na wahamiaji pamoja na kushirikiana majukumu kwa kundi kubwa la watu kwa kiwango cha dunia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon

Wakimbizi na wahamiaji hawatakiwi kuonekana kama mzigo, wanatoa fursa kubwa, kama tukiwafungulia kwa hilo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliuambia mkutano. Lazima tutekeleze haki za binadamu kwa wakimbizi na wahamiaji wote kwa nia yetu ya dhati.

Watu milioni 65 idadi ambayo haijawahi kutokea wamelazimika kukatisha maeneo mbalimbali duniani baadhi kutokana na mgogoro au manyanyaso, wengine kutokana na umaskini uliokithiri na wengi kutokana na majanga ya kiasili.

XS
SM
MD
LG