Taasisi ya Russia ya mamluki ya Wagner Group imejaribu kuandikisha baadhi ya vitengo vyake vilivyopo barani Afrika kwenda kupigana pamoja na Russia nchini Ukraine, afsa wa juu ya jeshi la Marekani barani Afrika ameiambia VOA.
“Tunaona baadhi ya juhudi za kuandikisha vitengo vya Wagner kwa ajili ya Ukraine,” Jeneral Stephen Townsend, kamanda wa kamandi ya Marekani Afrika, alisema katika mahojiano maalum na VOA wiki hii.
Townsend aliongezea kuwa vitengo hivyo huenda vikahamishwa kutoka Libya, ambako maelfu ya mamluki wa Russia wanamuunga mkono kamanda wa kijeshi Khalifa Haftar mwenye makao yake mashariki mwa nchi.
Townsend alisema AFRICOM imehamisha baadhi ya rasilimali zake kwenda kwenye kamandi ya Marekani huko Ulaya wakati Russia ilipoivamia Ukraine. Alisema kamandi imewapatia EUCOM kiasi cha wanajeshi 30, “wengi wao ni wachambuzi wa upelelezi na wapangaji,” pamoja na baadhi ya wanaohusika na upiganaji ili kushirikiana habari za kijasusi na upelelezi na ndege.
“Tumeona baadhi ya matokeo kwa mambo kama vile usafirishaji kwa ndege kwasababu tunaiimarisha NATO,” Townsend alisema.
“Pia tunafuraha ya kuipatia misaada kwa Ukraine, na hivyo hizo ndege zimepunguza baadhi ya mambo ya AFRICOM, lakini siwezi kusema kwamba walikuwa matokeo makubwa katika operesheni zetu,” amesema.
Mwez Januari, Townsend aliiambia VOA kuwa jeshi la Russia lilisaidia kwa kupeleka wanajeshi nchini Mali.
Hivi kuna takriban mamluki 1,000 wa Russia nchini Mali amboa wamefanya operesheni chache, alisema, lakini kundi hilo katika wiki za karibuni limeona msaada mchache kutoka kwa jeshi la Russia, pengine kwasababu ya uvamizi wake nchini Ukraine. Mamluki wa Wagner pia wako huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, na kwa kiwango kidogo nchini Sudan, alisema.
Townsend pia alisema anashuku kundi la kigaidi la al-Shabaab nchini Somalia huenda hivi sasa lina uwezo wa kuwashambulia wamarekani huko Afrika, ikiwemo nchini Marekani.
“Nashuku kwamba wanafanya hivyo. Hilo halikubaliki sana na Washington au katika jumuiya ya kipelelezi, lakini dhana yangu kama kamanda naamini wanafanya hivyo,” aliiambia VOA.
Hivi karibuni mwezi uliopita, maafisa wa Marekani walisema kwamba wakati washirika wa al-Qaida nchini Somalia wana utashi wa kuwalenga Magharibi nje ya Somalia, haina uwezo wa kuishambulia Marekani.
Townsend alikiri kuwa hafahamu uwezo wa kweli wa kundi hilo, na kusema uwezo ni kufanya mashambulizi dhidi ya maeneo ya nchini kwao ”hilo ni swali ambalo liko wazi.”
Alisema al-Shabaab imebakia kuwa “tishio kubwa” kwenye bara hilo, na katika muda wa mwaka mmoja uliopita, “limefurahia uhuru wa kutembea kote Somalia.”
“Wamepanuka zaidi, wenye nguvu na majasiri,” alisema.
Mwishoni mwa mwaka 2020, rais wa wakati huo Donald Trump aliamuru takriban wanajeshi 800 wa Marekani kuondoka nchini Somalia katika moja ya sera zake za mwisho za mambo ya nje akiwa madarakani. Takriban miezi 15 tangu wakati huo, majeshi ya Marekani yameendelea “kusafiri kwenda kazini,” wakiingia na kutoka Somalia kwa shughuli maalum wakati wakiwaacha wanajeshi wachache katika nchi hiyo iliyogubikwa na machafuko.
“Nadhani hakuna tija, kwa hakika haifanyi kazi vizuri. Hatuko huko muda mrefu wa kutosha kuongeza kasi, na halafu tukirejea tunaanza upya,” aliiambia VOA, akiongeza kwamba pia inaongeza hatari kwa wanajeshi wa Marekani ambao lazima wajiweka vyema kiusalama kila wakati wanapoingia na kutoka.
Akiulizwa kuhusu hali ilivyo na Seneta Mrepublican thom Tillis wakati wa kutoa ushuhuda kwenye kamati ya kijeshi, Townsend alisema, “tuko katika nafasi nzuri, tunaweza kurudi nyuma katika usalama nchini Somalia, katika hali ya ulinzi.”
Townsend aliiambia VOA aliamini Waziri wa Ulinzi, Lloyd Austin alitoa ushauri kwa White House na alikuwa akiupa utawala “muda na nafasi ya kufanya maamuzi.”
Townsend alisema mwez Januari kwamba Marekani iliamini kuwa China inajaribu kuweka kambi yake kwenye pwani ya Atlantiki huko Afrika, huku Equatorial Guinea kama sehemu ambako wachina walionekana kuwa wamekuwa na harakati nyingi,
Mwezi uliopita, Molly Phee, afisa wa juu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani anayeshughulikia Afrika, aliongoza ujumbe kwenda Equatorial Guinea ziara ambayo ilijumuisha wawakilishi kutoka AFRICOM.
“Viongozi huko Equatorial Guinea walikana vikali kwamba wana mpango wa kuwa na kituo cha kijeshi cha China nchini kwao. Kwa sasa tutaamini maneno yao, na tutaangalia wanachofanya,” Townsend aliiambia VOA wakati alipoulizwa kuhusu uhakikisho wowote ambao ujumbe ulipewa.
“Hatujaribu kuwaambia kwamba wachague kati ya Marekani na Magharibi na China,” alisema. “Isipokuwa ni vyema waheshimu wasi wasi wetu ulivyo katika usalama.”
China ina kituo chake pekee cha kijeshi nje ya nchi katika taifa dogo la Afrika Mashariki la Djibouti.
Townsend alisema mazungumzo kuhusu kambi ya kijeshi ya China nchini Tanzania yalipungua kasi kwa mabadiliko ya serikali ya Tanzania, kwahiyo China ilikuwa sasa “inajaribu kutafuta sehemu ya kuweka kambi yake,” huku nchi zote kwenye ukanda wa Msumbiji, ikijimuisha maji kwenye visiwa vidogo vidogo. China pia imefanya mazungumzo na serikali ya Somalia, ambayo, nayo ilitoa uhakikisho kwa Marekani kuwa haitakuwa na ushirikiano na jeshi la China, aliongezea.
Townsend pia alisema kuwa Iran ilihusika katika njama mwaka 2020 “ya kumuua balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini,” kufuatia shambulizi la anga ambalo lilimua kiongozi mkuu wa kikundi maalum cha ulinzi katika Jamhuri ya kiislamu ya Iran, Qasem Soleimani.
“Njama hiyo ilivurugwa,” alisema, akiongezea kwamba kulikuwa hakuna njama za karibuni za mashambulizi yaliyofanywa na Iran dhidi ya wamarekani barani Afrika.
Alisema kwamba maslahi ya Iran kwa Afrika yaliongezeka tangu mwaka 2020, huku Marekani hivi sasa ikiona kuibuka kwa drone za Iran kwenye bara hilo huku Tehran ikiendelea kutoa vifaa kwa mataifa ya Afrika.