Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 22:32

Juhudi za misaada ya kibinadamu Sudan zasonga mbele


Juhudi za kufanikisha misaada ya kibinadamu kwa mamilioni ya Wasudan zinasonga mbele lakini mazungumzo ya kusitisha mapigano bado yamekwama kwa sababu jeshi la Sudan, bado linakataa kutuma ujumbe kwenye mazungumzo ya amani yanayodhamiwa na Marekani, afisa wake anasema.

Mjumbe maalum wa Marekani kwa Sudan, Tom Perriello amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Jumatatu kwamba kutokana na udharura wa mgogoro wa Sudan, wajumbe kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Misri, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu wamekuwa wakifanyiakazi masuala yanayohusiana na usaidizi wa misaada ya kibinadamu na ulinzi wa raia.

“Pamoja na wadau wa masuala ya kibinadamu na wanadiplomasia kote ulimwenguni, sasa tuko kwenye ukingo wa Adre ukiwa wazi na zaidi ya malori 100 yakitarajiwa kuingia mapema kesho,” amesema.

Forum

XS
SM
MD
LG