Zikinukuu wakazi katika mkoa wa Sagaing, BBC idhaa ya Kiburma, Radio Free Asia (RFA), na gazeti la mtandaoni Irrawaddy, ziliripoti kuwa kati ya watu 50 na 100, wakiwemo raia walifariki katika shambulizi hilo.
Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha mara moja ripoti hizo na msemaji wa utawala wa kijeshi hakujibu ombi kwa njia ya simu kwa ajili ya kupata maelezo.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres alitoa taarifa akilaani vikali mauaji hayo na kutoa wito wa kuwajibishwa wahusika, msemaji wake amesema, akiongeza kuwa Guterres amerejelea wito wake kwa jeshi kusitisha kampeni ya ukatili dhidi ya wanainchi wa Myanmar nchini kote.
Jeshi lilikanusha tuhuma za kimataifa kwamba lilitekeleza ukatili dhidi ya raia na kusema linapambana na “magaidi” wenye dhamira ya kuyumbisha usalama wa nchi.