Maafisa hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe, wamewaambia waandishi wa habari kwamba Bilal al-Sudani, aliyetajwa na Marekani kama kiongozi wa ISIS nchini Somalia, aliuawa katika operesheni pamoja na washirika wake 10.
Wameongeza kuwa operesheni hiyo iliidhinishwa na Rais Joe Biden mapema wiki hii na kuendeshwa ndani ya saa 24 zilizopita.
Maafisa hao walikataa kutoa maelezo ya msingi kuhusu operesheni hiyo. Walikataa kuelezea tishio lolote la moja kwa moja lililosababishwa na Sudani kwa Marekani, ikiwa taarifa zozote za kijasusi zilikusanywa, jinsi jeshi la Marekani lilivyoendesha operesheni hiyo au ni wanajeshi wangapi walihusika katika operesheni hiyo.