Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:02

Jeshi la Israel limeripoti kuwauwa wanamgambo katika Ukanda wa Gaza


Wanajeshi wa israel wakifanya operesheni katika eneo la Khan Younis
Wanajeshi wa israel wakifanya operesheni katika eneo la Khan Younis

Wakati huo huo UN imesema mapigano makali katika eneo la Khan Younis yanawasukuma raia kusini zaidi kuelekea Rafah

Jeshi la Israel limeripoti Jumatatu kuwauwa wanamgambo kadhaa katika Ukanda wa Gaza wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akirudi katika eneo hilo kushinikiza sitisho jipyua la mapigano.

Jeshi la Ulinzi la Israel limesema operesheni zake katika siku moja iliyopita zilijumuisha mashambulizi ya anga na mapigano ya ardhini huko Khan Younis, kusini mwa Gaza, pamoja na mashambulizi kaskazini na katikati mwa Gaza.

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema mapigano makali katika eneo la Khan Younis yanawasukuma raia kusini zaidi kuelekea Rafah, ambako zaidi ya nusu ya wakazi wa Gaza tayari wamepatiwa hifadhi, wengi wakiwa katika makazi ya muda.

Umoja wa Mataifa unakadiria asilimia 75 ya wakazi wa Gaza wamekimbia nyumba zao, na inasema watu wa Gaza wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula, maji, makazi na dawa.

Pendekezo la kusitisha mapigano kwa muda litaongeza misaada ya kibinadamu kwa Gaza, pamoja na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas.

Forum

XS
SM
MD
LG