Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 30, 2024 Local time: 03:06

Jeshi la Bolivia laonyesha kutofurahishwa na hali ya kisiasa


Vikosi vya jeshi la Bolivia vimechukua uwanja wa kati wa mji mkuu Jumatano, na gari la kivita lilipita kwenye lango la ikulu ya rais likifuatwa na wanajeshi, na kuzua hofu ya mapinduzi ya kijeshi.

Rais wa Bolivia, Luis Arce, ameshutumu uhamasishaji usio wa kawaida wa baadhi ya vitengo vya jeshi mjini La Paz na kiongozi wa zamani Evo Morales, amemshutumu jenerali mkuu kwa kupanga mapinduzi.

Wanajeshi wenye silaha nzito na magari ya kivita walionekana wakikusanyika katika uwanja wa kati, Plaza Murillo, wakati shuhuda akiiambia Reuters kwamba ameona gari la kivita likiingia katika ikulu ya rais, ambayo iko kwenye uwanja huo na wanajeshi wakiingia ndani.

“Wakuu watatu wa majeshi wamekuja kueleza masikitiko yetu. Kutakuwa na baraza jipya la mawaziri, hakika mambo yatabadilika, lakini nchi yetu haiwezi kuendelea hivi tena,” Jenerali Juan Jose Zuniga amekiambia kituo cha televisheni cha nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG