Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:05

Jasusi wa Korea Kaskazini afunguliwa mashitaka Marekani


Waendesha mashtaka wa serekali kuu  wamemfungulia mashtaka afisa wa ujasusi wa kijeshi wa Korea Kaskazini kwa kula njama ya kupandikiza programu ya masuala ya kifedha kwenye mitandao ya watoa huduma za afya wa Marekani pamoja na NASA.

Mpango wake huo ulilenga pia kambi za jeshi za Marekani na makampuni ya kimataifa, kwa mashambulizi ya kuvuruga upelelezi wa mtandaoni.

Wizara ya sheria ya Marekani, Alhamisi ilimtambulisha raia wa Korea Kaskazini, Rim Jong Hyok kama afisa wa kitengo cha Andariel cha Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi ya Korea Kaskazini, ambayo maafisa wanasema inadhibitiwa na shirika la kijasusi la kijeshi la Korea Kaskazini.

Waendesha mashtaka wa serekali kuu wanasema Andariel alilenga vyombo 17 katika majimbo 11 ya Marekani, ikiwa ni pamoja na watoa huduma watano wa afya, wakandarasi wa ulinzi wa Michigan na California, kambi za jeshi na NASA.

Forum

XS
SM
MD
LG