Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Agosti 12, 2024 Local time: 19:10

Jaribio la wafungwa kuhepa gerezani limetibuka Somalia


Walinzi wa gereza wakiwa nje ya gereza kuu la Mogadishu. December 10, 2013.
Walinzi wa gereza wakiwa nje ya gereza kuu la Mogadishu. December 10, 2013.

Maafisa wa usalama wa Somalia wameharibu jaribio la wafungwa kutoroka gerezani leo Jumamosi katika mji mkuu wa Mogadishu.

Kulingana na vyanzo vya habari za uslama vimeambia VOA kwamba wafungwa waliokuwa wapiganaji, katika gereza kuu la Mogadishu, wakitumia bastola na guruneti, walishambulia walinzi wa gereza hilo.

Wafungwa hao wamefytua risasi dhidi ya walinzi na kulipua gruneti, kabla ya mashambuliano ya risasi kuanza.

Inaaminika kwamba silaha hizo ziliingizwa gerezani kwa njia ya magendo.

Maafisa wa usalama wamesema kwamba wamedhibithi hali katika gereza hilo na msemaji wa huduma ya magereza Abdiqani Mohamed Khalaf, ameambia waandishi wa habari kwamba walinzi watatu wa magereza wameuawa katika tukio hilo na wengine watatu kujeruhiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG