Idara ya utalii ya taifa hilo imesema kwamba makundi madogo ya watalii kutoka Australia, Singapore, Thailand na Marekani yatakubaliwa kuingia nchini humo baadaye mwezi huu.
Idara hiyo imeongeza kusema kwamba ziara hizo zitafuata ratiba na kuongozwa kila wakati na watalamu, huku watalii wakihitajika kuwa wamepatiwa chanjo kamili ya covid ikiwemo ile ya booster.
Watalii wa kigeni walizuiliwa Japan tangu mwanzoni mwa janga la corona mwaka 2020. Waziri mkuu Fumio Kishida kwenye hatuba yake mapema mwezi huu mjini London alisema kwamba atarekebisha kanuni za mipaka kuendana na mataifa mengine tajiri kufikia mwezi Juni,bila kutoa maelezo zaidi.