Kremlin ilipiga marufuku meli zisizo za Russia kuingia katika maji yaliyo karibu na visiwa vya Kuril – vinavyojulikana na Japan kama maeneo ya kaskazini – ambayo kwa sasa yanakaliwa na Russia lakini Japan inadai umiliki wake.
Tokyo inachukulia hatua hiyo kama sehemu ya vitisho kadhaa kutoka Moscow baada ya ushirikiano wa hivi karibuni kati ya Marekani na Japan.
Mapema mwaka huu, rais wa Russia Vladimir Putin alisema kwamba atavitembelea visiwa vya Kuril, hatua iliyopelekea kufifia kwa mazungumzo kuhusu umiliki wa visiwa hivyo vinavyozozaniwa na nchi hizo mbili.
Forum